NYOTA wa Manchester City, Mario Balotelli
amepanga kukutana na mwanamuziki Nicki Minaj Ijumaa wiki hii baada ya
kushindwa kuonana naye wiki iliyopita.
Mwanamuziki huyo atafanya shoo katika Ukumbi wa MEN Arena Jumaa hii
na Balotelli ambaye alilia kukutana naye bila mafanikio, atahakikisha
wanaonana.
Habari zinasema kuwa nyota wa Manchester City alitaka kukutana na
Nicki Minaj, lakini mwanamuziki huyo alikataa kwa kuwa alikuwa amechoka
na pia alikuwa na hasira.
Minaj alitumbuiza katika ukumbi wa News (MEN) Arena wiki iliyopita
na Balotelli aliwasili katika shughuli hiyo akiwa na rafiki zake.
Kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo alipanga kukutana na nyota
huyo kabla ya shoo lakini Minaj aligoma "Mario alisikitishwa na kitendo
hicho," alisema mtu wake wa karibu.
Imefahamika kuwa Mario mwenye miaka 21 alikuwa ameandaa kamera kwa
ajili ya kumpiga picha dada huyo lakini mambo hayakwenda vizuri.
Balotelli ni nyota katika soka lakini umaarufu huo haukutosha kumtoa ndani Minaj.
No comments:
Post a Comment