Baada ya mwishoni mwa wiki kuenea kwa kasi tetesi kuwa rais wa
manzese na kiongozi wa Tiptop Connection, namzungumzia Madee, kwamba
amejitoa kwenye kundi hilo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na
mmoja wa wasanii wa kundi hilo.
CHANZO CHETU kilifanya kazi ya ziada ya kumsaka msanii huyu ambapo alikanusha kuhusu tetesi hizo.
"Man jamaa wanaeneza tu story za uongo hakuna kitu kama hicho mimi
bado niko Tiptop kama kuna jipya lolote basi nitawajuza" alisema msanii
huyo.
Lakini hata hivyo chanzo chetu kilichopo karibu na wasanii wa kundi
hilo kilitudodosea kuwa ndani ya kundi hilo hivi sasa kuna matatizo
mengi mno tofauti na watu wanavyofikiri.
No comments:
Post a Comment