LIONEL Messi amethibitisha kuwa yeye ni bora
kuliko Pele. Nyota huyo wa Barcelona na raia wa Argentina, amempita
shujaa wa Brazil, Pele kwa kufunga mabao mengi kwa klabu na nchi yake
katika kipindi cha mwaka mmoja.
Messi alifunga mabao mawili kwenye mechi dhidi ya Mallorca wikiendi
iliyopita ambapo matokeo yalikuwa 4-2, hiyo ilimfanya afikishe mabao 76
mwaka huu, akiwa nyuma ya Gerd Muller kwa mabao tisa.
Muller ndiye anashikilia rekodi ya muda wote. Mchezaji huyo alifunga mabao 85 akiwa na Bayern Munich na Ujerumani mwaka 1972.
Messi ameipita rekodi ya Pele, ambaye alifunga mabao 75 akiwa kwenye kikosi cha Santos na Brazil mwaka 1972.
Lakini hiyo si mara ya kwanza kwa Messi kuvunja rekodi, msimu wa
2011/2012 alifunga mabao 73 na kuvunja rekodi ya mabao 67 iliyowekwa na
Mueller msimu wa 1972-73.
Vile vile Messi aliweka rekodi ya Ligi Kuu Hispania baada ya kufunga
mabao 50 msimu uliopita na alivunja rekodi ya Cesar Rodriguez iliyodumu
kwa miaka 57 kwa kutimiza mabao 232.
Kwa kutimiza mabao hayo, mchezaji huyo alikuwa nyota wa kwanza kufunga mabao mengi Barcelona.
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova alisema: Rekodi ya Leo ni nzuri.
Ni jambo zuri kuona amefunga mabao mengi. Kuna watu wanafikisha
idadi hiyo ya mabao baada ya kucheza mechi katika misimu saba au minane,
lakini yeye amefanya hivyo kwa mwaka mmoja. Na kitu kizuri ni kuwa
mabao yake mengi ni mazuri."
Messi, ambaye amekuwa akifunga mabao mawili kwenye mechi saba sasa,
amefikisha magoli 15 kwenye ligi. Vile vile ametimiza mabao 20 kwenye
michuano yote.
No comments:
Post a Comment