Habari za kuaminika kutoka katika klabu ya Azam ni kwamba imewasimamisha nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza kutokana madai ya kuchukua rushwa katika mchezo miwili ambayo timu hiyo ilifungwa na kulwa na doto wa soka la Tanzania.
Wachezaji ambao wametuhumiwa katika kesi wapo sita, lakini Said Morad, kipa Deogratius Munishi 'Dida' na kiungo Erasto Nyoni ndio ambao wamesimamishwa kuichezea Azam.
Chanzo cha kuaminika kutoka Azam kinasema kwamba, kuna wachezaji wengine watatu akiwemo nahodha Aggrey Morris na viungo wa kutumainiwa wawili wa timu hiyo nao wapo katika kesi hiyo, lakini kutokana na umuhimu wao katika timu imekuwa shida kidogo kuweza kuwasimamisha.
"Dida amesimamishwa kwasababu pengo lake litazibwa na Mwadini, wakati Saidi Morad nafasi yake yupo Owino, na pia Nyoni yupo dogo Nuhu. Hao wengine wameepuka adhabu ya kusimamishwa kwa sababu wataidhoofisha timu." - Kilisema chanzo hicho cha habari.
No comments:
Post a Comment