KAMATI
ya utendaji ya klabu ya Simba imewafuta uanachama viongozi na tawi
maarufu la Mpira Pesa, sambamba na kuzivunja kamati zake ndogondogo.
Mwenyekiti
wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage, amesema kamati ya utendaji ya Simba
iliyokutana juzi ilifikia maamuzi hayo baada ya kutokea kwa chokochoko
katika siku za hivi karibuni.
Alisema mwenyekiti wa tawi hilo,
Masoud Awadh na Katibu wake Ali Bane walikiuka katiba ya Simba kwa
kuongea hovyo na vyombo vya habari sambamba na kuitisha mkutano wa
wanachama bila ya kupata ruhusa ya uongozi.
Rage
aliongeza kuwa Awadhi si mwanachama hai wa klabu hiyo kutokana na
kutolipa ada ya uanachama kwa zaidi ya miaka miwili, huku barua yake
aliyouandikia uongozi kwa niaba ya Simba nayo ni kinyume na katiba
kwani hana mamlaka ya kufanya hivyo.
Tawi
la Mpira Pesa chini ya Awadhi lilifanya kikao cha kushinikiza Rage na
viongozi wenzake kuachia ngazi baada ya timu kufanya vibaya katika mechi
za mwisho za mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom na kuishia
nafasi ya tatu.
Kama hiyo haitoshi, wanachama wa tawi hilo waliorodhesha majina zaidi ya 600 ili kutimiza akidi inayoruhusu kufanyika kwa mkutano wa dharula wa Simba.
Hata
hivyo, Rage alisema uongozi umebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya
wanachama waliojiorodhesha ni wafu, huku pia saini zilizowekwa ni za
kughushi.
Kuhusiana
na kamati ndogondogo, Rage alisema uongozi umeona hazina msaada wowote
kwa timu hivyo hivi karibuni ataunda kamati nyingine zitakazosaidia timu
kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment