KOCHA Mserbia
wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi jana na sasa aliyekuwa kocha wa timu
hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari kutoka
ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni
kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya
nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak
amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart
atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka
Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya
Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
Bunjak mwenye
leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea
FC Damac ya Saudi
No comments:
Post a Comment