tuwasiliane

Tuesday, July 24, 2012

24 JUL.Milovan akunwa na Boban


Kwani umahiri aliotumia kufunga bao hilo la kusawazisha kwenye tmu yake, lilimfanya atamani kumpanga dakika zote 90.

Kauli hiy imekuja baada ya watoto hao wa Msimbazi 'Simba', kukabiliwa na mechi ya robo fainali ya Azam FC hapo Leo itakayowika ndani ya Uwanja wa Taifa, hapa Jijini.

Kwani lile bao la kiufundi lililofungwa na Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 66, kwenye mechi ya juzi dhidi ya Vita FC ya DR Congo, limemkuna kocha wake Milovan Cirkovic.

Kocha huyo alisema licha ya Boban kutokuwa fiti, hivyo kusita kumwanzisha, anatamani kufanya hivyo katika mechi ya kesho.

Alimmwagia misifa kwamba Boban ni mchezaji mzuri sana, ni mwenye umuhimu mkubwa katika timu, kinachofanya asimwanzishe ni kutokana na kuwa makini.

Alisema pamoja na changamoto hiyo, bado vijana wake watapambana kusaka ubingwa wa michuano hiyo huku akitoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti.

No comments:

Post a Comment