
KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, ameweka wazi kuwa mechi dhidi ya Azam FC ya robo fainali ya Kombe la Kagame leo Jumanne itakuwa ngumu, lakini amedokeza amenasa siri za wapinzani wake na ndizo atakazotumia kuwamaliza.
Simba na Azam zinavaana katika mechi itakayoanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo utatanguliwa na robo fainali nyingine kati ya AS Vita ya Jamhuri ya Congo na Atletico ya Burundi, ambayo pia inatazamiwa kuwa ya vuta nikuvute.
Mchezo huo wa Kombe la Kagame unazikutanisha Simba na Azam kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya mechi mbili za Kombe la Urafiki la Zanzibar.
Katika mchezo wa kwanza matokeo yalikuwa 1-1 lakini zilikutana tena fainali na Simba ilishinda kwa penalti.
Akizungumza na Mwanaspoti, Milovan alisema: "Mechi itakuwa ngumu kwa sababu Azam watakuja kwa nia ya kulipiza kisasi, lakini pia nitawakosa wachezaji wawili muhimu, Abdallah (Juma) na Kanu (Mbiyavanga), ambao ni wagonjwa.
"Pamoja na hali hiyo, Azam ni walewale wa kila siku, tumekutana nao mara nyingi sidhani kama kutakuwa na tofauti.
"Naijua vizuri Azam. Ninayajua vizuri mapungufu yao na uzuri wao.
"Kifupi naweza kukwambia Azam wanatisha zaidi upande wa kulia kwani wanapenda kuutumia katika kufanya mashambulizi."
Pia Milovan alisema wamerekebisha makosa waliyofanya kwenye mechi na AS Vita kwa kudai tatizo la mchezo ilikuwa sehemu ya kiungo.
"Hata hivyo uliona nilipomtoa, Kanu (Mbiyavanga) na kumwingiza Haruna Moshi `Boban' kipindi cha pili tulicheza vizuri zaidi," aliongeza Milovan.
Naye Stewart Hall ambaye atakuwa katika benchi la ufundi la Azam kuongoza timu yake, ambayo mechi mbili zilizopita ilikuwa chini ya msaidizi Kally Ongala, ameonya mchezo utakuwa mgumu.
"Mechi itakuwa ngumu kama unavyoijua Simba ni timu nzuri, lakini nasi ni wazuri pia, tutapigana kufa na kupona," alionya Stewart.
Simba huenda ikawatumia kipa Juma Kaseja, mabeki wa pembeni watakuwa Shamte na Shomari Kapombe wakati wa mabeki wa kati Juma Nyosso na Lino Masombo, viungo watapangwa Mwinyi Kazimoto, Mussa Mudde na Amri Kiemba wakati washambuliaji wanatazamiwa kuwa Felix Sunzu, Haruna Moshi `Boban' na Uhuru
source; gazeti la mwanaspoti
No comments:
Post a Comment