
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu mjini Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu wadhifa wake baada ya kuwepo kwa shinikizo la kuachia ngazi lilitoka kwa wananchi.
Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua
UPDATES
Kufuatia ajali ya meli ya MV SKAGIT waziri wa mawasiliano na miundombinu anayetokana na CHAMA CHA WANANCHI - CUF mhe. Hamad Masoud Hamad amewajibika kisiasa kwa kujiuzulu.
Taarifa zilizothibitishwa na ikulu ya zanzibar na kuthibitishwa na tv ya zanzibar ZBC jioni ya Leo zimeeleza kuwa mhe. Masoud alimuandikia rais wa zanzibar barua ya kujiuzulu tarehe 20/07/2012 na maombi yake ya kujiuzulu yamekubaliwa.
Kufuatia hali hiyo rais wa zanzibar amemteua mwakilishi wa jimbo la Ziwani kwa tiketi ya CUF, mhe. Rashid Suleiman Seif kuwa waziri mpya wa wizara hiyo.
Mhe. Masoud amefanya like ambalo limewashinda CCM kwa miaka mingi. Namchukulia kama kiongozi mzalendo kwa hatua ya kuwajibika.
Hapa ndio kila kitu blog itakuletea taarifa zaidi baadae
No comments:
Post a Comment