
MABAO mawili ya mshambujliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Herman Tcheche,
jioni hii yametosha kuivusha Azam FC hadi fainali ya Kombe la Urafiki, baada ya
kuwafunga mabingwa wa Zanzibar, Super Falcon 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Tcheche alifunga bao la kwanza dakika ya 67, akiunganisha krosi ya Hamisi Mcha wakati bao la pili, alifunga kwa penalti, dakika ya 77, baada ya Samir Haji Nuhu kuangushwa kwenye eneo kla hatari na Samir Said dakika ya 77.
Kwa matokeo hayo, Azam inasubiri mshindi wa mechi kati ya Simba SC na Zanzibar All Stars, mechi inayoanza saa 2:00 usiku huu Uwanja wa Amaan kucheza naye fainali keshokutwa.
Katika mechi hiyo, Azam ilipata pigo dakika ya 54, baada ya mshambuliaji wake Gaudence Exavery Mwakimba kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 54 kwa kumpiga kiwiko Abdul Ally.
No comments:
Post a Comment