
Kwani inatarajia kutumia mechi hiyo, kuipima timu yake inayotarajiwa kuanza kutetea ubingwa wa Kombe la kagame, kuanzia siku ya Jumamosi ndani ya Uwanja wa Taifa hapa Jijini.
Si wengine bali ni wale Mabingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga, siku ya kesho wanatarajia kulitawala dimba kwa dhumuni la kuikabili JKT Ruvu katika mechi yao ya kirafiki itakayochezwa saa 10:30 kwenye Uwanja wa Taifa hapa jijini.
Mabingwa hao watatumia mechi hiyo kuipima timu yake, inayotarajia kuanza kutetea ubingwa wa Kombe la Kagame kuanzia Jumamosi kwa kuivaa Atletico ya Burundi.
Naye Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema kwamba kocha wao mpya, Tomo Saintief atapata nafasi ya kuwaona wachezaji wake katika mechi kwa mara ya kwanza baada ya kutua katika klabu hiyo wiki iliyopita.
Mratibu wa mchezo huo, Salum Mkemi, alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na klabu zote ziko tayari kwa mechi hiyo ambayo pia itatumiwa na ‘maafande’ kujiandaa kwa ligi kuu ya Bara itakayoanza Septemba.
Mbali na hilo viingilio kwenye mechi hiyo katika viti vya kijani kuwa ni Sh. 3,000, wakati viti vya rangi ya chungwa ni Sh. 5,000 na sehemu nyingine za viti vya rangi ya bluu vilivyobakia ni Sh. 10,000.
No comments:
Post a Comment