tuwasiliane

Monday, July 9, 2012

09 JUL.Cheka afungiwa na TPBO


Baada ya Francis Cheka kumkimbia Japhet Kaseba katika uwanja wa taifa siku ya sabasaba, wasimamizi wapambano hilo TPBO wamemfungia Cheka kwa kitendo hicho.

TPBO imemfungia bondia huyo toka 'mji kasoro bahari' Morogoro kwa kutofanya naye kazi, wala kutoa kibali chochote cha pambano la aina yoyote linalo muhusu Cheka.

Cheka ambaye anasemekana hana mpinzani ndani ya Tanzania katika tasnia ya ngumi za kulipwa, alitakiwa kuutetea ubingwa wake mbele ya Japhet Kaseba, ambapo mara ya mwisho kukutana Kaseba alipigwa na Cheka.

No comments:

Post a Comment