

Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka amelazwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa katika pori la Pande nje kidogo ya jiji akiwa taaban.Inasemekana Dk Ulimboka alitekwa jana na watu wasiojulikana.
Kwa taarifa zaidi ungana nasi baadaye
SOURCE; MWANANCHI
NEW UPDATE
Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums, Dk Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye 'face to face' kwa ajili ya mazungumzo.
Tukio hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo mengine huduma zimeendelea kama kawaida
BLOG HII ITAENDELEA KUWAPA UPDATES ZAIDI
No comments:
Post a Comment