tuwasiliane

Wednesday, June 27, 2012

27 JUN.MCHEZAJI AFIA UWANJANI NCHINI UGANDA


Mashabiki wa mpira wa miguu huko Sironko Uganda wamepata mshituko baada ya mchezaji kuzimia kwenye uwanja wa mpira na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.

Simon Musika ana umri wa miaka 30 na alicheza kwenye hiyo mechi ya timu za mitaani kwa dakika 15 kabla ya kuzimia na kufariki dunia ambapo baada ya taarifa za kifo chake ilibidi mechi isimamishwe.

Ndugu wa marehemu walikusanyika kwenye uwanja wa mpira muda mfupi tu baada ya kifo cha mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment