
Habari hizo za uzushi zilikuwa zikienezwa na mwanadada kuhusu msanii huyo, kwamba anaksana na wasanii wenzake.
Siku za usoni akiwa kwenye mishemishe zake za hapa na pale, alipigiwa simu akijulishwa kwamba kuna habari zimezagaa kwneye Radio pamoja na mitandao baadhi juu ya maisha yake huku zingine zikivuma kwamba amepokonywa gari aina ya BMW.
Hayo yalisemwa kwa Mwigizaji Nyota kwenye sanaa ya Filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper, amefunguka kwa kusema kuwa kuna mtangazaji mmoja ambaye amekuwa akitumia nafasi yake kwa kumpiga vita na kumzushia kashifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujaribu kumtengenezea mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike.
Wolper alisema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa gari yake aina BMw X 6 kuwa amenyeang,anywa.
Mwanadada huyo amesema kuwa yeye ana gari zaidi ya moja, kwa hiyo hakuna mtu wa kumpangia atembelee gari gani.
Kwani katika taarifa hizo ilisemekana kuwa kuwa alikuwa kitembelea gari aina ya Noah yaani gari yake ya awali, akiongea zaidi alisema kuwa habari za kumchafua zimekuwa zikitengenezwa na mwanadada mmoja ambaye ni mtangazaji lakini akasema kuwa hana sababu ya kumtaja kwani anajijua.
No comments:
Post a Comment