Naye Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa mazoezi ya Cirkovic yatawika mishale ya saa 10:00 jioni.
Lengo la mazoezi hayo ni kujiweka tayari kwa mashindano ya Kombe la Kagame yanayotarajiwa kushirikisha timu zaidi ya 12 kutoka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na timu zitakazoalikwa kutoka katika maeneo mengine ya ukanda huo.
Naye Kocha wa timu hiyo ya Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, alisema siku ya leo mishale ya saa 10:00 jioni, ataanza kukisuka upya kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa kwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayowika hapa Jijini kuanzia Julai 14 hadi 29.
Kocha huyo alirejea nchini juzi usiku akitokea kwao, ambako alikwenda likizo baada ya msimu wa ligi uliopita kumalizika Mei 6 mwaka huu.
Kamwaga alisema ujio wa kocha huyo utawasaidia kurekebisha upungufu ulioonekana, katika mechi mbili za kirafiki zilizofanyika walizocheza hivi karibuni katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Pindi kikosi hicho kikiwa Kanda ya Ziwa, kilionyesha kiwango cha juu na wana imani kwamba watafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, na HATA katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Kocha huyo alisema anataka kukutana na wachezaji uwanjani hapo kesho saa 10:00 na moja kwa moja, ataendeleza mazoezi kwa sababu hata kile ambacho walikuwa wanafanya chini ya msaidizi wake (Amatre Richard) kilitokana na maelekezo yake.
.
No comments:
Post a Comment