tuwasiliane

Monday, June 25, 2012

25 JUN.Okwi kwenda Italia Julai 4


Mshambuliaji tegemeo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba, Emmanuel Okwi, anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kuelekea Italia kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio na timu mbalimbali zinazoshiriki ligi ya Serie A ya nchini humo.

Hata hivyo, tayari Simba imeshakubaliana na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini kwa dau la Euro 550,000 (sawa na Sh. bilioni 1.07) endapo nyota huyo atashindwa kupata timu huko Italia.

Okwi ambaye alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Uganda (Cranes) bado yuko Kampala na atarejea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii ili kukamilisha taratibu za safari.

Akizungumza jana na gazeti hili, Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa Okwi atakuwa Italia kwa muda wa wiki mbili na atakuwa chini ya wakala ambaye aliwasiliana na Simba kwa ajili ya kumtafutia timu mshambuliaji huyo.

Kamwaga alisema kuwa Simba imefurahi kuona kuwa nyota ya mchezaji huyo imefunguka na ndio malengo yake kuona inatimiza ndoto za wachezaji wake kupata timu zinazoshiriki katika ligi zilizoendelea.

Alisema pia Simba inajipanga kuhakikisha inasajili wachezaji watakaoziba nafasi ya nyota walioondoka na waliowaacha ili waweze kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa ambayo watashiriki.

Simba pia imeshapokea maombi kutoka kwa Orlando Pirates ya Afrika Kusini ikitaka kumfanyia majaribio mshambuliaji huyo mw

No comments:

Post a Comment