tuwasiliane

Saturday, June 9, 2012

09 JUN.Maximo kurithi mikoba ya Papic


Wengi walikuwa wakimpiga madongo huku wengine wakisikika wakisema kwamba hafai....Kwa mara nyingine tena anatua ndani ya Jiji la Bongo kwa dhumuni la kuja kuwanoa watoto wa Jangwani 'Yanga'.

Si mwingine bali ni yule aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Marcio Maximo anatarajia kuwasili nchini wiki ijayo na kuchukuwa mikoba ya Kocha aliyekuwa anamaliza muda wake kwenye Klabu hiyo ya Yanga.

Alisema ujio wake si wapekeyake bali anaambatana na kocha msaidizi wa Viungo, huku akiwa ameongozana na mkewe kutokana na kuwa nashughuli pevu ya kukiandaa kikosi hicho cha Yanga kinachotarajia kushiriki michuano ya Kombe la Kagame.

Mara tu baada ya kupokea maombi ya kukinoa kikosi hicho Maximo hakuwa na pingamizi lolote bali alikubaliana na maombi hayo moja kwa moja huku akitoa mapendekezo ya kuwasajili wachezaji awatakao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Katika mapendekezo hayo ya wachezaji aliowahitaji Maximo ni pamoja na Beki wa Simba, ambaye hadi sasa bado anazua gumzo na mtafaruku mkubwa baina ya Klabu hizo mbili za watani wa jadi Simba na Yanga, Kelvin Yondan, pamoja na Kipa Ali Mustapha 'Bartez'.

Aidha imeelezwa kuwa Kipa huyo anayehitajika na Kocha mpya Maximo, 'Bartez' tayari amekwisha saini mktaba na Klabu hiyo, huku Kipa namba tatu wa timu hiyo, Shaban Kado, akiachiwa kwa Mkopo kurejea katika kikosi cha timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment