tuwasiliane

Saturday, June 9, 2012

09 JUN.Lady Jay Dee live Mwanza


Ni ile siku iliyokuwa ikingojewa kwa hamu sana na mashabiki wa mwanamuziki huyo, ndani ya Nyerere Hall Gold Crest Hotel jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 20,000/- tu kwa kila atakayeingia.

Mmmh! Siyo lazima uhadithiwe jitose mwenyewe na mkwanza wako, ukamshuhudie mwana dada
Lady Jay Dee akiambatana na Machozi Band huku akisimama na Barnaba na Bendi yake.

Ni Leo Jumamosi ya Juni 9 mwaka huum , uje ukiwa umependeza na kujipatia mafotozi kwa Blogs, Facebook na Twitter.

Mbali na wanawake hata wanaume wanakaribishwa kujumuika Leo, ikiwa ni pamoja na kucheza magoma makali na mwanamuziki Barnaba huku tukipaza sauti za kiitikio cha Magube-gube....Usikose chalii wangu ukayarudi magoma hayo ndani ya Jiji la Mwanza.

No comments:

Post a Comment