
Alisema mara nyingi mavazi yanategemea sana na sehemu husika hata kama mtu ukiwa star yaani nyota, huwezi kwenda kanisani na kimini.
Sehemu ambazo hazistahili kwa mavazi yaliyo tofauti, unatakiwa kuvaa vazi linalostahili na inafikia mahali lawama inawaangukia sana wasanii wakionekana kama ndivyo wavaavyo.
Hayo yalisemwa na Msanii nyota wa Filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper Massawe ‘Jack’ , alisema kwamba mara nyingi suala la mavazi utegemea na tukio ama sehemu husika tofauti na watu wanavyofikiria kwamba msanii akiwa katika mavazi fulani eti ndiyo mavazi yake ya kila wakati kitu ambacho si kweli.
Wolper alisema ni vigumu ukienda sehemu fulani kama Disco, huwezi kuvaa vazi lisilohusika na sehemu uendayo.
Alimalizia wka kusema kwamba kuna nguo huvaliwa kwenye filamu tu na mtu huwezi kuvaa vazi la filamu ukiwa mtaani, kwani wasanii ni sehemu ya jamii jambo amabalo hata jamii inatakiwa walione kwa sababu kunawatu si wasanii na wana viwalo 'nguo' vya ajabu.
No comments:
Post a Comment