Friday, April 20, 2012
20 APR. Julio arejea CDA
Mchezaji wa zamani wa CDA pamoja na Simba SC, Jamhuri Kihwelo 'Julio', anataraji kurejea kwenye timu yake iliyomlea na kumtambulisha kwenye ramani ya Soka la Bongo CDA kama kocha wa timu hiyo.
Julio anataraji kukaa kwenye benchi la ufundi la CDA yenye maskani yake Dodoma, katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu anayoifundisha kwa sasa Coastal Union mchezo utakao chezwa jumamosi hii.
Julio akizungumza na Uhuru FM alisema, mchezo huo utakao maalum kwa ajili ya kuiaga Coastal Union ambayo ameinusuru na janga la kushuka daraja na kurejea nyumbani CDA.
"Nitakaa kwenye benchi la Coastal kwa dakika 45 za kwanza, na 45 nyingine nitakuwa kwenye benchi la CDA katika mchezo huo," alisema Julio ambaye pia ni kocha msaidizi katika kikosi cha Kilimanjaro Stars (Timu ya Taifa ya Tanzania Bara), Serengeti Boys (timu ya Taifa ya chini ya miaka 17) na ni kocha wa timu ya taifa ya soka la wanaume ya olimpik (u23).
Julio alipata kutamba na CDA katika miaka yake ya uchezaji, na sasa anarejea kuhakikisha CDA inarejea Ligi kuu ya Vodacom na kwa sasa inajianda na ligi ya Taifa ngazi ya Taifa inayotaraji kukata utepe hivi karibuni.
Dodoma haitakuwa na timu katika Ligi kuu msimu ujao baada ya Polisi Dodoma kuwa katika hali mbaya ya kushuka daraja na inahitaji miujiza ya Mungu kubakia Ligi kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment