Friday, April 20, 2012
20 APR. OKWI; SIMBA KAZI NI KAZI TU
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi amesema wana jukumu moja ya kuhakikisha wanafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza baada ya kumalizika mchezo dhidi ya JKT Ruvu, Okwi alisema kazi kubwa mbele yao kwa sasa ni mechi zake za kimataifa kwani ubingwa wa Ligi Kuu kwa asilimia kubwa upo mikononi mwao.
Mwishoni mwa mwezi huu, Sima itakuwa na mchezo dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan kwenye Uwanja wa Taifa kabla ya kurudiana ugenini."Jambo la msingi kwa sasa ni wachezaji wote kuendeleza ushiriano waliokuwa nao tangu mwanzo ili kuthibitisha kwa Watanzania kuwa hawakubatisha kufika hapo," alisema Okwi.
Naye kocha timu hiyo, Mserbia Curkovic Milovan alisema mechi za Ligi Kuu walizocheza ni kipimo tosha cha maandalizi yao kabla ya kuivaa Al Ahly."Tunahitaji kutumia vizuri michezo hii ya ligi kama sehemu ya maandalizi yetu ya mechi inayokuja ya Afrika."
Wakati huohuo, Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kambi ya timu hiyo imehama toka Bamba Beach na kwenda Sunfire hoteli na mazoezi watakuwa wakifanya katika Uwanja wa Sigara.
Simba yenye pointi 56 kibindoni, itakutana na Moro United siku ya Jumatatu katika mwendelezo wa mechi zake za Ligi Kuu litakalopigwa saa moja usiku kwenye uwanja wa Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment