tuwasiliane

Wednesday, April 18, 2012

18 APR. Shughuli nzito Barca, Chelsea leo


KOCHA wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri amesema kikosi hicho hakina sababu ya kuiogopa mabingwa watetezi Barcelona watakapokutana kwenye mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo.
"Wameshakutana kwenye mechi kadhaa kabla ya Andres Iniesta kufunga bao katika dakika za majeruhi, lakini hadithi inaweza kuwa tofauti safari hii."

Itakuwa mara ya tano kwa timu hizo kukutaka katika hatua ya mtoano ya michuano hiyo, na inaweza kurejesha kumbukumbu wakati Iniesta alipofunga bao muda mfupi kabla ya filimbi ya mwisho kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kuipeleka hatua nyingine Barcelona.

Barca inapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele hatua ya fainali, lakini Ranieri anadhani kwamba , kocha wa muda wa 'Blues', Roberto di Matteo ana mbinu za kuivusha timu hiyo pekee ya England kwenye michuano hiyo.
"Siyo rahisi eti kwa sababu tu Barcelona ni timu bora duniani kwa sasa," alisema Ranieri. "Wachezaji wake wengi wako kwenye kiwango kizuri kwa sasa.

"Hapa siyo suala la kumsimamisha Messi kwa sababu Barca haiundwi na Messi tu. Kuna Xavi, pia kuna Iniesta. Wana wachezaji wengi wazuri, lakini piat Chelsea ina wachezaji kadhaa wazuri kutoa ushindani," alisema.

Wakati Ranieri akisema hayo, Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona, Andoni Zubizarreta amesema analiona pambano la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Soka Ulaya leo dhidi ya Chelsea ya England kama sehemu ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Real Madrid (Clasico) mwishoni mwa wiki hii.

Barcelona iko nyuma kwa pointi nne dhidi ya mahasimu wao Real Madrid kwenye msimamo wa Ligi Kuu Hispania, huku wakijiandaa kuwakaribisha vinara hao kwenye uwanja wao wa nyumbani, Camp Nou Jumamosi jioni.
Bacelona inawinda kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa Ulaya tangu AC Milan ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1990.

Zubizarreta anaona kuwa mechi dhidi ya Chelsea ni nyepesi lakini inaweza kuwa sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Real Madrid."Mechi dhidi ya Blues kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, ni sehemu ya maandalizi ya 'Clasico'. Hii ni wiki ya mlipuko. WAKATI HUO HUO NUSU FAINALI YA KWANZA JANA USIKU ILISHUHUDIWA REAL MADRID WAKIPATA KICHAPO CHA GOLI 2-1 KUTOKA KWA BAYERN MUNCHES MAGOL YA BAYEN YALIFUNGWA NA FRANK RIBBERY KATIKA KIPINDI CHA KWANZA NA GOMES KATIKA DAKIKA ZA LALA SALAMA. GOLI LA KUFUTIA MACHOZI LA MADRID LILIFUNGWA NA RONALDO

No comments:

Post a Comment