Duh! nimewahi kuhadithiwa jinsi watu watu wanavyomiminika kwenye misiba ya watu maarufu pamoja na ya viongozi, ila huu sikukubai hata kuhadithiwa niliamua kwenda kushughudia mwenyewe..ni ukweli ni kwamba msiba uliogusa mioyo ya watu wengi kama huu wa Steven Kanumba.
Watu wengi wamehuzunika na si hapa Tanzania tu bali hata nje ya nchi mbalimbali zinazozunguka nchi ya Tanzania Afrika nzima na hata Ulaya.
Binafsi sikujua kama Kanumba alikuwa maarufu kiasi hichi na sipati picha kama Mungu angempa miaka mingine 28 ingekuwaje? Embu jiulize hapo.
Umati ambao ulianza kukusanyika kuanzia siku aliyokufa na kufanya hadi vituo vya mbalimbali vya Radio kutangaza kuwa, watu wasiendelee kwenda nyumbani kwake ambako kulisababisha hata barabara kufungwa na kusababisha hata polisi kulazimika kuweka ulinzi mkali kuanzia nyumbani kwake.
Lakini kilichotia fora ni umati ambo umejitokeza kumuaga na kusababisha hata baadhi ya barabara kufungwa leo wakati wa shughuli za kumuuaga watu wengi wamezimia hata kusababisha hata viwanja ambavyo vilidhamiwa vitafaa Leaders kuwa ni mahali padogo hata kuhatarisha usalama wa watu na kusababisha ratiba ya mazishi kubadilishwa ili kuondoa msongamano wa watu ambao nao ungeweza kusababisha maafa mengine.
Ukiachilia umati huo wa watu lakini kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakifuatilia tukio hilo kwa njia ya TV mbalimbali/Radio na Internet ili woote wanje ya Tanzania waweze kushuhudia tukio hilo.
Niliweza kuonge na msanii wa filamu za Kibongo anayejulikana sana na wale wapenzi wa filamu hizo za hapa nyumbani Mzee Chilo juu ya kifo cha mwanasanaa mwenzao Steven Kanumba alisema kwamba wameumia sana kwa mwenzao kuwatoka kwani wamepoteza nuru katika sanaa ya Filamu za Kibongo.
Alisema kwamba wakiwa kama wasanii wa Filamu za Tanzania, yawapasa kumpelekea Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete malala miko yako katika sanaa hiyo hasa.
Alisema enzi za uhai wa marehemu Steven Kanumba aliweza kuigiza Filamu zaidi ya 40 mpaka hapo mauti ulipomkuta.
Steven Kanumba aliweza kufyatua filamu zaidi ya 40 enzi za uhai wake, mpaka pale mauti ilipomfika.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba....Ametangulia nasi tuko nyuma tukimfuata kwani safari ni ya wote...Amina.
No comments:
Post a Comment