Wednesday, April 11, 2012
11 APR. SIMBA VS TP MAZEMBE
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta na Patrick Ochan watakutana tena na wachezaji wenzao wa zamani, viongozi wao- kwa ujumla na timu ya zamani, Simba SC.
Katika kuhakikisha Simba inazidi kuimarika kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mfanyabiashara maarufu na mwanamichezo Azim Dewji anakusudia kuileta nchini timu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa ajili ya kuipa makali Simba kabla ya wawakilishi hao wa Tanzania hawajaivaa Al Ahly Shandy ya Sudan.
Dewji aliyeifadhili Simba kwa miaka mingi, alisema jana Dar es Salaam kuwa ziara inaratibiwa na kampuni yake ya Simba Trailers na kwamba ameshazungumza na kuafikiana na Rais wa Mazembe, bilionea Moise Katumbi Chapwe na pia uongozi wa Simba.
“Pamoja na kuwazawadia pesa wachezaji wa Simba, nimeona nitoe mchango zaidi kwa kuwaletea mechi ya kujipima nguvu na timu bora ya Mazembe ya
Kongo,” alisema Dewji aliyetoa sh milioni 15 kwa Simba baada ya kuitoa ES Setif ya Algeria.
Kwa mujibu wa Dewji, mchezo baina ya Mazembe na Simba unatarajiwa kufanyika Aprili 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni wiki moja kabla ya `Wekundu wa Msimbazi’ kuumana na Al Ahly.
Alisisitiza kuwa, Mazembe itakuwa kipimo sahihi kwa Simba kutokana na kuwa na kikosi chenye hadhi ya juu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment