
Azam na Simba wameendelea kufukuzana baada ya timu zote kushinda katika michezo yao ya ligi kuu Tanzania Bara hii leo.
AZAM STADIUM
Azam FC waliwakaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi na mpaka timu hizo zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa Azam FC ambapo Mrisho Khalfan Ngassa akichukua nafasi ya Ibrahim Mwaipopo.
Haikuchukua mda kwa Ngassa kuziona nyavu za Ruvu Shooting kwani dakika ya 49 aliipatia Azam FC goli pekee la Ushindi.
JAMHURI MOROGORO
Wakata miwa wa Manungu Mtibwa Sugar wameendelea kuwa mboga kwa Simba kufuatia ushindi wa goli 2-1 walioupata Simba hii leo katika uwanja huo wa Jamhuri.
Simba SC walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Patrick Mutesa Mafisango katika dakika ya 19 kufuati kazi nzuri ya Emmanuel Okwi na Haruna Moshi 'Boban'.
Goli hilo la Simba lilidumu mpaka dakika ya 52 ambapo Hussein Javu aliipatia Mtibwa Sugar goli pekee katika mchezo huo.
Goli hilo lili waamsha Simba na dakika ya 57 walipata penati iliyopigwa na Patrick Mafisango na kuchezwa vyema na kipa wa Mtibwa Deo Munish 'Dida'.
Ulikuwa ni wakati mwingine kwa Mzambia Felixs Sunzu kuibuka shujaa wa Simba baada ya kuifungia Simba goli la pili katika dakika ya 70. Na mpaka mwisho wa mchezo Simba 2-1 Mtibwa Sugar
MATOKEO MENGINE
TOTO AFRICAN 2 - 1 POLISI DODOMA
No comments:
Post a Comment