
Ile chenji ya rada, zaidi ya Sh bilioni 75 sasa imeiva na wakati wowote itakuwa mikononi mwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) baada ya Hati Maalumu ya Makubaliano (MoU) baina ya pande zinazohusika kusainiwa.
Hati hiyo ilisainiwa jana kati ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya Uuzaji wa Silaha ya Uingereza (BAE System), Ofisi ya Uingereza ya Kupambana na Ufisadi (SFO) na Idara ya Kimataifa ya Misaada ya Maendeleo (DFID).
Taarifa iliyofika mezani kwetu jana ilieleza kuwa fedha hizo na riba yake, zitatumika kwenye elimu kwa mujibu wa makubaliano baina ya Serikali za Tanzania na Uingereza, na matumizi hayo yatafuatiliwa kwa makini ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment