
*Asema Ababuu kamponza, laiti angejua...
HUKU madai ya kubeba mimba nje ya ndoa yakisambaa mithili ya moto wa kifuu, nyota wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amelifungukia Ijumaa na kusema kuwa, anajuta kufahamiana na kijana anayeitwa Ababuu kwa kuwa ndiye chanzo cha yote yanayosemwa.
Uwoya aliyefunga ndoa na msukuma kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ juzikati alisema kitendo cha yeye kuwa na ukaribu na kijana huyo ndicho kilichowafanya wabaya wake waibue ishu ya kuwa ni mjamzito na mhusika si mwingine bali ni huyo Ababuu.
“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish, alidai amekuwa karibu na Ababuu kwa mambo ya kawaida tu, wala hawakuwa wapenzi kama wengi walivyovumisha.
“Wabaya wangu wameitumia fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.
Je, mimba anayo?
Kila alipokuwa akiulizwa kuhusu kubeba ujauzito, Uwoya amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha na hivi karibuni alipokutana na mwandishi wetu licha ya kitumbo chake kuonekana kimetuna alisema: “Wewe unanionaje kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya ndoa.”
Katika siku za hivi karibuni, Uwoya amekumbwa na skendo ya kudaiwa kubeba ujauzito nje ya ndoa huku mhusika akitajwatajwa kwa jina la Ababuu ambaye ni mpenzi wa zamani wa msanii wa filamu, Jacqueline Wolper.
Hata hivyo, licha ya mashosti zake kutoa ushuhuda kuwa anavyoonekana ana kibendi, kila alipoulizwa amekuwa akichenga kuzungumzia ishu hiyo.
SOURCE GLOBAL PUBLISHERZ
No comments:
Post a Comment