tuwasiliane

Sunday, March 18, 2012

18 MARCH. YANGA 1 VILLA SQUAD 0


Kwa mara nyingine tena mshambuliaji toka Uganda Hamisi Kiiza kuwatoa mabingwa wa Tanzani Bara na Afrika Mashariki na Kati Dar Young African 'Yanga' salama katika uwanja wa Taifa.

Yanga leo walikuwa wageni wa Villa Squad katika muendelezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara katika uwanja wa Taifa, na iliwachukua dakika 89 kuziona nyavu za Villa squad, kupitia kwa Hamisi Kiiza.

Kipa wa Villa Squad alifanya kazi ya ziada kuokoa hatari langoni mwake na kuwafanya washambuliaji wa Yanga kuonekana butu kwa dakika hizo 89. Yanga walipoteza nafasi kadhaa kupitia kwa Kenneth Asamoah.

Katika kipindi cha Kwanza Villa Squad nusura wapate goli la kuongoza lakini umakini hafifu wa safu yake ya ushambuliaji walipoteza nafasi hiyo. Mpaka mwisho wa mchezo Yanga 1-0 Villa Squad.


Mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom uliwakutanisha Coastal Union ya Tanga na JKT Oljoro ya Arusha katika uwanja wa Mkwakwani wa Tanga na mchezo kumalizika kwa Coastal Union kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Goli la Coastal Union lilifungwa na Said Sued kwa njia ya mkwaju wa penati katika dakika ya 18 ya mchezo.


Ligi hiyo inatarajia kuendelea Kesho kwa michezo minne katika mikoa minne:
TOTO AFRICAN Vs POLISI DODOMA, CCM Kirumba Mwanza
AZAM FC Vs RUVU SHOOTING, U/azam Chamanzi Dar es salaam
MTIBWA SUGAR Vs SIMBA SC, Jamhuri Morogoro

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (20) 44
2. Yanga SC (20) 43
3. Azam FC (20) 41
4. Mtibwa Sugar (20) 34
5. Coastal Union (21) 29
6. JKT Oljoro (22) 28
7. JKT Ruvu (20) 27
8. Kagera Sugar (21) 24
9. Ruvu Shooting (20) 24
10. African Lyon (18) 18
11. Moro United (21) 18
12. Toto Africa (20) 17
13. Polisi Dodoma (21) 17
14. Villa Squad (20) 16

No comments:

Post a Comment