tuwasiliane

Tuesday, March 13, 2012

13 MARCH.Kajumulo sasa AUTAKA uongozi TFF!


Mdau wa soka aliyepata kumiliki timu ya soka ya Sigara, Alex Kajumulo amesema anakusudia kuwania uongozi katika Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Akizungumza katika kipindi cha michezo ya kituo kimoja cha Radio cha jijini Dsm, Kajumulo anayeishi nchini Marekani alisema kama Mtanzania anapaswa kuwania uongozi katika klabu hiyo na amepata msukumo huo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa viongozi wa soka la Bongo.

"Nitajitosa kugombea moja ya nafasi katika uchaguzi ujao wa TFF....ila sitarajii kugombea urais, nafanya hivyo kwa lengo la kutaka kuiweka pazuri soka ya Tanzania kupitia mimi kuwa ndani ya uongozi,"Alisema Kajumulo.

Pamoja na michezo Kajumulo ambaye pia ni mfanyabiashara, amejitosa katika tasnia ya muziki akiimba mtindo wa Reggae.

No comments:

Post a Comment