tuwasiliane

Thursday, March 1, 2012

01 MARCH. Simba, Etech kuingia mkataba


UONGOZI wa klabu ya Simba leo unaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech kwa ajili ya kufungua tovuti (website) itakayokuwa ikitoa taarifa zote zinazoihusu klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa wameamua kuingia mkataba ili wapenzi wa timu hiyo wapate habari kwa uharaka kupitia tovuti hiyo baada ya ile ya mwanzo kutofanya kazi katika kiwango kizuri na kuamua kuifunga.

Alisema kupitia tovuti hiyo uongozi wa Simba unaamini wapenzi wa klabu hiyo watapata habari zinazohusu timu hiyo kwa uharaka zaidi na kwa muda wowote sambamba na kutoa maoni yao juu ya maendeleo ya timu yao.

"Kuanzia Machi 1 Simba itaingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Etech, ambapo itafungua tovuti kwa ajili ya kupata habari za klabu yetu kwa uharaka na kwa muda unaotakiwa, lengo hasa ni kurahisisha mawasiliano kati yetu na wadau wetu, ambapo tutakuwa tukienda kisasa zaidi,"alisema Kamwaga.

Aidha katika hatua nyingine Kamwaga alisema kesho kutakuwa na uzinduzi wa kipindi cha Simba TV ambacho kitakuwa kikirushwa moja kwa moja na televisheni ya Clouds ambacho kitakuwa kikionyesha matukio mbalimbali ndani ya klabu hiyo yakiwamo matukio yanayoihusu klabu hiyo tangu ilipoanza mpaka ilipofikia hivi sasa.

Alisema tayari tiketi kwa ajili ya uzindizu wa kipindi hicho zimeanza kutolewa katika makao makuu ya klabu hiyo ambapo kila moja inauzwa 70,000 na uzinduzi huo utafan

No comments:

Post a Comment