tuwasiliane

Thursday, March 1, 2012

01 MARCH.Nassari kuibeba CHADEMA Arumeru!


Mgombea wa kura za maoni kuwania kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameibuka mshindi wa kura hizo.

Nassari ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu uliopita na marehemu Jeremiah Sumari, aliibuka kidedea katika kura hizo zilizopigwa jana katika eneo la Maji ya Chai baada ya kujizolea kura 808 kati ya kura 888 zilizopigwa.

Wengine waliojipima ubavu naye na kura zao katika mabano ni Anna Mghwira (23), Anthony Musani ambaye alitoka CCM baada ya kushindwa kura za maoni na kujiunga Chadema aliambulia kura nane, Godlove Temba (18), Rebeca Magwisha (12), Samweli Shamy (10) na Yohane Kimuto aliyeambilia kura sita.

Awali Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, alitamba kuwa chama hicho kitashinda katika uchaguzi huo kwa kuwa kina sera za kisanyansi zinazozingatia mambo yanayohitajika na wananchi.

Alisema hakuna kulala mpaka kieleweke Arumeru na kusisitiza kuwa hata mafisadi wakimwaga fedha Chadema wanatumia mbinu ya kisanyansi zaidi kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment