tuwasiliane

Monday, February 27, 2012

27 FEB. YANGA KUKWEA PIPA ALHAMISI WIKI HII


Kwani hakutakuwa na Mashabiki Uwanjani, kutokana na Zamalek kutumikia adhabu ya kucheza mechi bila mashabiki kwa muda wa mwaka mmoja iliyopewa Aprili 20 mwaka jana.

Na ilipewa na Bodi ya Nidhamu ya CAF kutokana mashabiki wake kufanya fujo kwenye mechi ya michuano hiyo mwaka jana ilipocheza dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Si wengine bali ni wale Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara 'Yanga', itaondoka nchini aiku ya alhamisi kuelekea Cairo kwa dhumuni la mechi yao ya marudiano ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zamalek itakayowika siku ya Jumamosi ndani ya Uwanja unaomilikiwa na jeshi la Misri.

Naye Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Louis Sendeu, alisema kuwa wameamua kuondoka siku hiyo ili kikosini wawe pamoja na nyota wao walioko kwenye timu ya taifa (Taifa Stars) ambayo keshokutwa itakuwa inamenyana na Msumbiji kwenye mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Alisema kikosi kinachotarajiwa kuondoka hakitakuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na kile kilichocheza mchezo wa kwanza hapa Jijini.

Kwani maandalizi ya safari hiyo yako katika hatua za mwisho, kwa sababu waliamini mchezo huo utafanyika Cairo licha ya kuiomba CAF ibadilishe uwanja kutokana na sababu za kiusalama.

"Idadi kamili ya wachezaji watakaoondoka mwalimu (Kostadin Papic) amesema ataiweka wazi Jumatano, kuna wachezaji wengine wako Stars hivyo pia anahitaji kujua maendeleo yao kabla ya kuchagua silaha atakazoondoka nazo," aliongeza Sendeu.

Mbali na hilo hakuna mchezaji majeruhi kwenye kikosi hicho sasa na mazoezi yanaendelea kila siku jioni kwenye uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika.

Aliongeza kuwa mbali na wachezaji, pia viongozi kadhaa wanatarajiwa kuambatana na timu hiyo bila kuzidisha idadi ya watu 40 iliyoelezwa na CAF katika barua yake.

Mechi hiyo ya Zamalek na Yanga itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba ni Gihed Greisha wa Misri huku Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga kutoka Tunisia.

No comments:

Post a Comment