tuwasiliane

Friday, February 3, 2012

03 FEB.diamond ampotezea mwandishi


Wiki moja baada ya kumuandikia barua kali msanii DIAMOND barua ambayo inamtaka msanii huyo kumlipa shilingi milioni 30 mwandishi Fransic Godwin wa Iringa kama fidia baada ya kumpiga na kumuharibia vifaa vyake pamoja na kumdhalilisha, mwanasheria wa mwandishi huyo amesema mpaka sasa DIAMOND hajajibu chochote baada ya kupokea barua hiyo.

Mwanasheria huyo Paul Lekamoi amesema bado mwimbaji DIAMOND ana wiki nyingine mbili za kuhakikisha analipa kiasi hicho cha fedha la sivyo watakwenda kumshitaki katika levo za juu zaidi za kimahakama, ambapo mpaka sasa Diamond hajapatikana kuzungumzia chochote kuhusu barua aliyoandikiwa.

Chanzo cha hii ishu kufika ilipo ni kutokana na mwandishi wa habari kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama ya mwanzo Iringa, ambayo ilimaliza kesi ya DIAMOND kwa kumuamuru msanii huyo kulipa faini isiyozidi laki moja kwa mahakama na kwa mwandishi huyo kama fidia, uamuzi ambao haukumpendeza mwandishi huyo.

No comments:

Post a Comment