tuwasiliane

Friday, February 3, 2012

03 FEB. KHADIJA KOPA YUKO TAYARI KUPATA MTOTO!


Malkia wa muziki wa TAARAB TANZANIA mwimbaji KHADIJA KOPA ambae atatatimiza umri wa miaka 49 may mwaka huu, ameamplfy exclusive on millardayo.com kwamba yuko tayari kupata mtoto wa mwisho.

amesema”mume alienioa sasa hivi maskini bahati mbaya alikua na mtoto mmoja tu na akafariki, kwa hiyo Mungu akama atanipa mtoto sasa hivi nitamshukuru ili na Mume wangu apate ukumbusho, ikiwa sasa hivi itakua sawa manake umri nao unakwenda”

Khadija kopa ni mama wa watatu, alikua na watoto wa nne lakini mtoto wake wa kwanza Omari alifariki dunia.

kwa kumalizia Khadija ameamlfy kwamba “mtoto wake wa kwanza Omari alipata na mume mwingine, watoto wangu wengine wawili nimepata na mume mwingine, na huyu wa mwisho nimezaa na mume mwingine,… ehhhhhh sikai na magume gume baba mie”

sasa hivi Khadija anaishi na mume mwingine ambae wameoana miaka mitano iliyopita, ambae bado hawajabahatika kupata mtoto.

SOURCE millardayo.com

No comments:

Post a Comment