tuwasiliane

Tuesday, October 4, 2011

4 oct Siwahitaji:Ferdinand, Defoe walia na Capello

Mmoja ya wachezaji ambao hawaitajiki na Capello, Rio Ferdinand
LONDON, ENGLAND
JERMAIN Defoe na Rio Ferdinand hawamo katika kikosi cha kocha wa England, Fabio Capello kitakachocheza mechi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Ulaya dhidi ya Montenegro, Ijumaa wiki hii.

Miezi sita iliyopita Ferdinand alikuwa nahodha wa England na Defoe ambaye ameanza kasi kwa kufunga mabao matatu katika mechi nne zilizopita, ameshangaa kwa nini hajaitwa. Mchezaji huyo wa Tottenham alisema: "Nimekosa amani baada ya kutemwa." �Naamini sijawahi kumwangusha Capello wakati nilipocheza, lakini nitafanya kila niwezalo kuhakikisha ninapata nafasi kwa mara nyingine."

Ferdinand, ambaye ameitwa katika timu ya taifa mara 81 tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza chini ya kocha Glenn Hoddle, Novemba 1997, alikuwa nahodha mpaka alipopoteza nafasi mbele ya John Terry, Machi mwaka huu.
Iliaminika kuwa angeitwa katika kikosi baada ya kupona matatizo ya misuli.

Lakini pia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 aliingia kipindi cha pili katika mechi dhidi ya Norwich, ambayo ilitazamwa na Capello.

Capello aliamua kumwacha nyota wa Liverpool, Steven Gerrard baada ya kutokea mvutano na kocha Kenny Dalglish, ambaye anaona kwamba Gerrard hastahili kuingia katika timu ya taifa kwani ndio kwanza amepona maumivu yaliyokuwa yakimsumbua.

Ijumaa iliyopita, Gerrard alikiri kuwa hakutaka kuingia katika timu ya taifa kwa kuwa anaona hajapata mazoezi ya kutosha.
Capello alimuita mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck na kipa wa zamani wa West Brom, Scott Carson. Pia alimtaja Bobby Zamora kwa mara ya kwanza tangu alipokosekana katika timu ya taifa mwaka jana kufuatia

No comments:

Post a Comment