MSHAMBULIAJI wa Simba, Uhuru Suleiman, amefunguka na kuweka wazi kilicho moyoni mwake kwa kusema Nadir Haroub �Cannavaro� wa Yanga ndiye mfalme wa nafasi ya beki ya kati kwa Tanzania na hana mpinzani.
Uhuru ametamka hilo kwa maelezo kuwa amefanya utafiti wake kama mshambuliaji kwa miezi 13 akiwaangalia mabeki tofauti katika michuano mbalimbali iliyopita.
Akizungumza na na mwandishi wetu, Uhuru alisema; "Tanzania kuna mabeki wengi, lakini kwa sasa hakuna kama Cannavaro, na kwamba huyo ni zaidi ya wote utake, usitake."
"Mimi ni mshambuliaji, najua beki gani wa kuogopwa, kumpita Cannavaro lazima ufanye kazi kubwa na ndiyo maana nasema, Tanzania kwa sasa hana mpinzani, wengine watafuata, naamini ninachokizungumza na hii ni baada ya utafiti wangu wa miezi 13 sasa."
Cannavaro, ambaye pia huchezea Zanzibar Heroes, aliitwa dakika za mwisho kwenye kikosi cha Taifa Stars na kufanya mazoezi ya siku moja kabla ya kuondoka na kuelekea Morocco kwa mechi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika baada ya Victor Costa kuumia nyonga.
Akizungumzia hilo, Uhuru alisema kuwa;" Haijalishi, lakini ieleweke kuwa anastahili kuwepo na kama asingekuwepo, kungekuwa na pengo kubwa.
No comments:
Post a Comment