KINDA la Simba, Shomari Kapombe amewapa raha mashabiki wa timu hiyo, baada ya kumwambia kocha wake, Moses Basena amtumie atakavyo ili amfanyie mambo.
Hii ni dalili nzuri kwa simba kuwa imelamba dume baada ya kumsajili nyota huyo kutoka Polisi Morogoro ambaye sasa ni kipenzi cha mashabiki kutokana na kiwango na uimara wa kumudu namba nyingi uwanjani.
Kocha Basena amekuwa akimtumia kwa nafasi tofauti uwanjani kulingana na timu wanayocheza nayo, kiungo na beki, kwa nafasi zote amefanya vizuri na kuwa simulizi mechi inapomalizika.
Aliliambia Mwanaspoti kuwa: ��Mimi sina tatizo, kocha anipange nafasi yoyote, kulingana na chaguo lake, mwenyewe atafurahi. Nina kipaji cha kucheza kwa ufasaha namba zote isipokuwa kipa, namba tatu na 11 naweza japokuwa si sana,��alisema Kapombe aliyeweka wazi namba tano (sentahafu) ndiyo anaipenda zaidi.
Aliongeza kwa kusema, kwa sababu Simba ni timu kubwa ushindani ni mkubwa, lakini atajituma ili apate nafasi ya kumudu kikosi cha kwanza.
source
mwanaspoti
No comments:
Post a Comment