tuwasiliane

Sunday, September 3, 2017

MLEWA LODGE KIWANJA MATATA SANA NDANI YA KILOSA.KARIBUNI SANA


MLEWA LODGE NDANI YA KILOSA


MANCHESTER CITY KUICHUKULIA HATUA ZA KISHERIA ARSENAL

Image result for sanchez
Arsenal na Manchester City zilifikia makubaliano ya kuuziana Alexis Sanchez kwa kitita cha paundi milioni 60 lakini Wenger aligeuza kibao baadaye
Manchester City inataka kuichukulia Arsenal hatua za kisheria baada ya kuzuia uhamisho wa Alexis Sanchez siku ya kufungwa dirisha la usajili wa majira ya joto.
Miamba hao wa Manchester inaaminika walifikia makubaliano ya paundi milioni 60 na Arsenal kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mapema Alhamisi asubuhi, lakini hakuna kilichofanyika.
Arsenal waliamua kubatilisha makubaliano hayo baadaye siku hiyo baada ya kumkosa Thomas Lemar, ambaye aliamua kubaki Monaco kwa msimu mwingine.
Kwa mujibu wa chanzo cha Chile El Murcurio, sakata hilo la uhamisho halijaisha bado kwani City wanataka maelezo ya kina ni kwa nini waligeuziwa kibao na wanataka kwenda mbele zaidi.
Habari nyingine tofauti imedai kuwa Sanchez hajafurahia tabia ya Arsenal kipindi chote cha majira ya joto na yupo tayari kufanya mgomo, ingawa Arsene Wenger alitia maji madai hayo akisisitiza Ijumaa kwamba mchezaji huyo bado ana mapenzi na klabu kwa asilimia mia moja.

“Magoli mawili niliyowafunga Botswana yatanisaidia Morocco” – Msuva

Simon Msuva amesema magoli mawili aliyofunga kwenye mechi dhidi ya Botswana yatamsaidia kujiamini katika klabu yake ya Difaa El Jadid pindi atakaporejea Morocco.
Msuva amecheza katika kiwango cha juu dhidi ya Botswana na kufanikiwa kutumia vizuri nafasi alizozipatakupachika mabao yaliyoipa Stars ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wa nyumbani.
“Magoli mawili niliyofunga kwenye timu ya taifa yataniongezea kujiamini na kwenda kufanya vizuri kwenye klabu yangu lakini nitaendelea kuaminika kwenye timu kwa sababu unapocheza kwenye timu ya taifa na kufunga wanaona huyu mchezaji anaweza kutusaidia,” Simon Msuva.

SIMBA YAIOGOPA AZAM FC,YAOMBA GAME YAO KUSOGEZWA MBELE KISA OKWI


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo linatarajiwa kutoa ratiba mpya ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyofanyiwa marekebisho na ndani yake mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliokuwa ufanyike Septemba 6 umesogezwa mbele hadi Septemba 9.

Na hatua hiyo inafuatia maombi ya klabu ya Simba kutaka mchezo huo usogezwe mbele kwa kuwa wachezaji wake wawili tegemeo, beki Juuko Murshid na mshambuliaji Emmanuel Okwi hawatakuwepo.Wawili hao wapo na timu yao ya taifa, Uganda ambayo inajiandaa kwa mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia mwakani Urusi dhidi ya wenyeji, Misri Septemba 5. Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo, Agosti 31 Uganda walishinda 1-0 mjini Kampala.

Hata Uganda wakiondoka Cairo siku moja tu baada ya mchezo hakuna namna Juuko na Okwi wanaweza kuwahi mechi na Azam jioni ya Septemba 6, hivyo TFF imeusogeza mbele mchezo huo hadi Septemba 9.
Na TFF imeiagiza Bodi ya Ligi kuhakikisha haipangi mechi wakati wa ratiba za michezo ya kimataifa, kuepuka mambo kama ambayo yanasababisha mechi ya Azam na Simba kusogezwa mbele.Nicholas Gyan ataondoka kurejea klabu yake, Ebusua Dwarfs ya kwao, Ghana ili kukamilisha taratibu za uhamisho wake.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Hans Poppe amesema 
kwamba, Gyan alilazimika kuja kushiriki tamasha la Simba Day ambalo ni maalum kwa utambulisho wa wachezaji wapya, lakini leo anarejea Ghana.
Hans Poppe amesema kwamba Gyan anamaliza mkataba wake Agosti 20, mwaka huu Ebusua Dwarfs na baada ya hapo atarejea nchini – maana yake anaweza kuiwahi mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Yanga Agosti 23, mwaka huu.

Wakati huo huo: Mshambuliaji mpya, Nicholas Gyan amerejea jana asubuhi Dar es Salaam tayari kuanza rasmi maisha mapya katika klabu yake mpya aliyojiunga nayo mwezi uliopita kutoka Ebusua Dwarfs ya kwao, Ghana.
Gyan aliondoka nchini Agosti 9 baada ya kutambulishwa Simba SC katika tamasha la Simba Day Uwanja wa Taifa kurejea Ghana kukamilisha taratibu za uhamisho wake na baada ya kufanikisha hilo, tayari yupo nchini.
Wachezaji wengine wa kigeni Simba SC kiungo Mghana, James Kotei, beki Mzimbabwe na Nahodha Method Mwanjali, kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na mshambuliji Mrundi, Laudit Mavugo.

Serena Williams ajifungua mtoto wa kike

Bingwa wa tennis kwa upande bi Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika hospitali moja ya mjini Florida Marekani.
Bingwa wa tennis kwa upande bi Serena Williams amejifungua mtoto wa kike katika hospitali moja ya mjini Florida Marekani.
Japo mwenyewe na jamaa zake hawajatoa tangazo rasmi tayari kuna ujumbe wa kumpa hongera katika ukurasa rasmi wa Twitter akaunti ya US Open Tennis kutoka kwa kocha wake miongoni mwa wengine .
Itakumbukwa mwanamama huyo aliweka rekodi ya kushinda kinyanganyiro cha Australian Grand Slam kwa mara ya 23 mwaka huu January, japo alishindana akiwa mja mzito.
Serena alikiri kwamba alifichua kuhusu mimba yake kwa ulimwengu kimkosa mnamo mwezi Aprili baada ya kupakia picha katika Intagram kimakosa katika mtandao wa Snapchat.
Alishinda taji la Australian Open mnamo mwezi Januari akiwa mjamzito na katika taarifa yake katika jarida la Vogue mwezi uliopita alisema kuwa anataka kutetea taji hilo.

Barcelona: Liverpool ilihitaji £183m kumuuza Coutinho

Phelippe Coutinho
Barcelona imesema kuwa liverpool iliitisha £183m kwa uhamisho wa nyota wake Phillipe Countinho katika siku ya mwisho ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho siku ya Ijumaa.
Liverpool wamekataa maombi matatu kutoka kwa mabingwa hao wa Uhispania kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikuwa ameomba uhamisho.
''Liverpool ilikuwa inataka Yuro milioni 200 na kwa kweli hatungeweza kukubali hilo'', alisema mkurugenzi wa Barcelona Albert Soler.
Tunamshukuru mchezaji huyo kwa juhudi alizofanya , kwa sababu alijaribu sana na kutuonyesha kuwa alitaka kuichezea Barcelona.
Soler ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumamosi aliongezea: Hali ilimalizika ilivyomalizika na hakuna chengine tunachoweza kufanya.
Barcelona ilimtaka Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa PSG kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha £200m.
Liverpool imesema kuwa Coutinho hauzwi na kukataa maombi ya £72m, £90m na jingine la £114m kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Uhispania ambalo lilifungwa siku moja baada ya lile la Uingereza kufungwa.
Coutinho aliyefunga mabao 14 msimu uliopita na kuhudumia miezi sita akiwa na jeraha la kifundo cha mguu aliweka kandarasi mpya ya miaka katika uwanja wa Anfield mnamo mwezi Januari.

Saturday, September 2, 2017

Rooney akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Rooney atafikishwa mahakamani baadae mwezi huu
Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney amekamatwa na baadae kuachiliwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa, polisi mjini Cheshire imesema.
Rooney alikamatwa baada ya polisi kusimamisha gari aina ya Volkswagen Beetle ambayo alikuwa anaendesha.
Polisi wa Cheshire wanasema Rooney mwenye miaka 31, ana mashtaka ya kujibu kwa kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa na akiwa pia kwenye mwendo mkali.
Nahodha huyo wa zamani wa England na Manchester United ameachiliwa, lakini kesi yake itasikilizwa baadae mwezi huu.
Rooney ambaye amestaafu soka la kimataifa mwezi uliopita, ndiye anashikilia rekodi ya ufungaji mabao muda wote kwenye timu ya taifa akiwa na magoli 53.
Alijiunga tena na klabu yake ya utotoni Everton, miaka 13 baada ya kuondoka Merseyside kwenda Manchester United.

Saturday, August 26, 2017

MANCHESTER UNITED KULIAMSHA DUDE TENA DHIDI YA LEICESTER CITY LEO JUMAMOSI?

Romelu Lukaku has made a huge impact since his arrival, but his nose may be put out of joint
Manchester United watakuwa wenyeji wa Leicester City Leo Jumamosi baada ya kushinda 4-0 mara mbili mfululizo kwenye mechi za mwanzo Ligi ya Uingereza.
Foxes watasafiri mpaka Old Trafford baada ya kuanza msimu kwa mwendo wa wastani, lakini litakuwa jaribio gumu kwa Leicester kupata matokeo mbele ya vinara wa ligi.
Mechi ya Jumamosi itakuwa ni 125 baina ya pande hizo mbili, United wakiwa wameshinda 63 ikilinganishwa na mechi 33 walizoshinda Leicester City

Azam FC full mzuka kuikabili Ndanda leo

WAKATI kikiendelea na mazoezi ya mwisho kabla ya kuuanza msimu mpya kwa kukabiliana na Ndanda, kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kipo kamili kabisa kuelekea mchezo huo.
Mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utafanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara kesho Jumamosi kuanzia saa 10.00 jioni.
Kikosi hicho tayari kimewasili mkoani Mtwara tokea juzi na jana kilifanya mazoezi ya kwanza mkoani humo, huku leo Ijumaa saa 10.00 jioni kikitarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja huo utakaohodhi mtanange huo.
Wachezaji wote wa Azam FC waliokuwemo kwenye msafara wa timu, wako kwenye hali nzuri na morali ya juu tayari kuanza mapambano ya kuwania taji la ligi hiyo.
Habari njema kuelekea mchezo huo, ni kikosi hicho kutumia jezi mpya kabisa za msimu huu, ambazo watazizindua rasmi kwenye mtanange huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa aina yake kutokana na upinzani wa pande zote mbili.
Katika kujiandaa na msimu huu, Azam FC imecheza jumla ya mechi 10, ikishinda tano, sare tatu na kufungwa miwili huku ikifunga jumla ya mabao 16.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita, ilianza kwa kupiga na mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports na kupoteza kwa jumla ya mabao 4-2, kabla ya kutoka suluhu na Mbeya City, ikapoteza kwa kufunga 2-0 na Njombe Mji lakini ikailaza Lipuli ya Iringa mabao 4-0, mechi hizo tatu ikicheza Nyanda za Juu Kusini.
Iliporejea jijini Dar es Salaam, ikailaza KMC bao 1-0, bao pekee likifungwa na Nahodha Msaidizi Aggrey Morris, kwa njia ya mkwaju wa penalti baada ya Wazir Junior kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Baada ya mchezo huo, kikosi hicho kikaenda kumalizia mechi za majaribio nchini Uganda kwa kambi ya siku 10 na kutoka sare mabao 2-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), ikatoka sare nyingine ya 1-1 na Mabingwa wa Uganda KCCA kabla ya kuzichapa URA (2-0), Onduparaka (3-0) na Vipers (1-0).
Ingizo jipya
Azam FC inaanza msimu mpya wa ligi ikiwa na baadhi ya sura mpya, ambazo ni za wachezaji vijana wenye vipaji, ambao baadhi yao wametoka kwenye kituo cha kukuza vipaji cha timu hiyo ‘Azam FC Academy’ kama vile mshambuliaji anayekuja vizuri Yahya Zayd, kiungo Bryson Raphael, Swalehe Abdallah (Majimaji), Joseph Kimwaga, kipa Benedict Haule (Mbao FC)
Wachezaji wengine wapya walioongezwa kwenye kikosi hicho ni Mchezaji Bora Chipukizi wa msimu uliopita, Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), mshambuliaji Wazir Junior, beki wa kushoto Hamimu Karim (Toto Africans), Idd Kipagwile (Majimaji) na kipa Mghana Razak Abalora (WAFA FC).
Pamoja na usajili huo, pia safari hii Azam FC imepata kibali cha Uhamisho wa Kimataifa (ITC) cha kumtumia winga wake, Enock Atta Agyei, ambaye alishindwa kutumika msimu uliopita kwenye mechi za mashindano rasmi hapa nchini baada ya kutokuwa na umri wa miaka 18 (aliotimiza Desemba mwaka jana) sambamba na kibali hicho.
Ingizo la wachezaji hao, limeonekana kuimarisha kikosi hicho ambacho kimeonekana kufanya vizuri sana katika mechi zake za mwisho za maandalizi nchini Uganda.
Washambuliaji wake, Yahaya Mohammed, Yahya Zayd na Wazir Junior, wameonekana kufanya vizuri kwenye maandalizi hayo katika eneo la kucheka na nyavu, hali ambayo inaleta matumaini ya kikosi hicho kunufaika na mabao msimu huu kutokana na ukali wa safu yake.
Huku pia washambuliaji wengine Mbaraka Yusuph aliyetoka kwenye majeruhi na Shaaban Idd, anayeendelea na matibabu wakitarajiwa nao kufanya makubwa kwenye eneo hilo pale watakapokaa sawa na kuwa fiti tayari kwa ushindani.
Rekodi zilipokutana Ndanda vs Azam FC (Head to Head)
Kihistoria kwenye mechi za ligi timu hizo zimekuwa na upinzani mkali, ambapo Azam FC imekutana na Ndanda mara saba (sita VPL na mara moja kwenye FA Cup).
Katika mechi hizo Azam FC imeshinda mara nne, mara tatu ikiwa kwenye ligi na mara moja kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) huku Ndanda ikishinda mara mbili na mchezo mmoja ukiisha kwa sare.
Jumla ya mabao 15 yamefungwa kwenye mechi hizo zote (ukiwa ni wastani wa mabao mawili kila mechi), Azam FC ikiwa imefunga tisa, na Ndanda ikifunga sita.
Mara ya mwisho msimu uliopita kwenye mchezo uliofanyika uwanja huo, Azam FC inayodhaminiwa na maji safi ya Uhai Drinking Water yanayokata kiu yako, Benki ya NMB na Tradegents, ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1, lakini ziliporudiana Azam Complex, matajitri hao walishinda 1-0 bao lililofungwa na Yahaya Mohammed kufuatia pande safi la juu la Nahodha Himid Mao ‘Ninja’.