tuwasiliane

Tuesday, August 8, 2017

Kaseke aitabiria makubwa Singida United

Deus Kaseke wa Yanga na Juma Mahadhi wa Coastal Union
Kiungo wa Singida United Deusi Kaseke, ameitabiria 
mambi makubwa timu hiyo, kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.
Kaseke aliyetokea Yanga, alisema kiwango kilichoonyeshwa na timu yao kwenye mchezo wa kirafiki waliocheza juzi dhidi ya Yanga, ambapo licha ya kufungwa lakini waliweza kuwamudu mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu.

Kaseke amekiambia chanzo chetu, kama wataendelea kucheza kwa kiwango hicho anaamini msimu ujao watakuwa ni moja ya timu zinazopigania ubingwa wa ligi hiyo.
“Inapendeza kuona tunacheza vizuri na kutoa ushindani kwa timu kubwa kama Yanga, unajua ni muda mfupi tangu tumekaa kambini kujiandaa na msimu mpya lakini tumeonyesha nini tunataka,”amesema Kaseke.

Kiungo huyo mkabaji alisema  wataendelea kujifua huku wakifuata maelekezo ya makocha wao anaamini hadi ligi itakapoanza watakuwa fiti na wanaweza kufikia malengo yao ambayo wameyakusudia.
Kaseke amesema walipofikia kwenye maandalizi yao siyo pabaya sana na kitu cha msingi hapo wanatakiwa kucheza mechi nyingi za kirafiki ili kuweza kuzoeana zaidi jambo ambalo litawasaidia kupata matokeo kwenye mechi zao.
Singida United tayari imecheza mechi saba za kirafiki na haijafanikiwa kushinda hata mchezo mmoja zaidi ya kutoka sare na kufungwa.

No comments:

Post a Comment