Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez amelazimika kubaki Emirates hadi msimu ujao wa majira ya joto baada ya kukosa timu inayotaka kumsajili
Alexis Sanchez atamaliza mkataba wake wa miezi 12 iliyobaki Arsenal kabla ya kuondoka Emirates mwisho wa kampeni za 2017-18.
Mkataba wa Sanchez utafika mwisho msimu ujao wa majira ya joto, na inafahamika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile amekataa kufanya mkataba mpya na Washika Mtutu.
PSG imetajwa kumfukuzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini miamba hao wa Ligue 1 wamemsajili Neymar kwa rekodi ya dunia, Bayern Munich nao wakiwa wameamua kuacha kumfuatilia.
Arsene Wenger amekataa kumuuza Sanchez kwa wapinzani wake Manchester City, na kwa mujibu wa The Mirror, mshambuliaji huyo atalazimika kupambana na hali yake.
Ripoti zimedai kuwa Sanchez hataki kubaki Arsenal zaidi ya msimu ujao wa majira ya joto, lakini amejipanga kuitumikia kuitumikia Arsenal katika kampeni za 2017-18, kabla ya kuondoka kama mchezaji huru Juni 2018.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, ambaye amefunga mabao 30 katika mechi 51 msimu uliopita, alishuhudia mechi ya Arsenal dhidi ya Chelsea jukwaani katika uwanja wa Wembley Jumapili mchana.
No comments:
Post a Comment