Kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba cha msimu uliopita amesema anahisi mambo yatakuwa tofauti msimu ujao baada ya klabu hiyo kumsajili Emmanuel Okwi raia wa Uganda.
Simba imemsajili Okwi mchezaji anayekubalika sana kwenye klabu ya Simba hivyo ujio wake unaweza kumweka Kichuya katika wakati mgumu wa kupata namba endapo Mganda huyo atakuwa kwenye kiwango chake kinachofahamika.
Kichuya mshindi wa tuzo ya mfungaji wa bao bora la msimu uliopita ameiambia Goal, hofu yake nikwamba huenda kocha Omog, akampa nafasi zaidi Okwi na yeye kusota benchi kwasababu ya yeye ni mzawa.
“Hiyo ndiyo hofu Yanga naweza nikaanza msimu kwa kuanza kikosi cha kwanza lakini ikitokea mechi mbili tatu sijacheza vizuri nitaondolewa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi akapewa Okwi, “ amesema Kichuya ambaye pia ndiyo alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo kwa msimu uliopita.
Winga huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar, alisema hofu hiyo inamjia kwasababu vitu kama hivyo vimeshawakuta baadhi ya wachezaji wenzake ambao licha ya juhudi kubwa walizozifanya lakini baadaye walishindwa kuthaminiwa kwenye timu ambazo walizipigania na kuzipa mafanikio.
Kichuya ni mmoja wa wachezaji waliochangia Simba kutwaa taji la Kombe la FA na kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu yaTanzania Bara, kutokana na juhudi alizokuwa akizionyesha uwanjani.
No comments:
Post a Comment