tuwasiliane

Friday, July 28, 2017

ARSENAL HAIJAKATA TAMAA KUMSAJILI KYLIAN MBAPPE

Image result
Arsenal haijafanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu lakini hawajakata tamaa kuinasa saini ya Mbappe sawa na Madrid na City
Imeripotiwa kuwa Arsenal bado wanalo tumaini la kukamilisha usajili wa winga wa AS Monaco, Kylian Mbappe licha ya kudaiwa kuwa mchezaji huyo anakaribia kutua Real Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ameingia kwenye rada za klabu kubwa za Ulaya majira ya joto kufuatia mafanikio makubwa aliyopata kampeni za msimu uliopita, alipofunga jumla ya magoli 26 katika michuano yote na kuisaidia Monaco kutinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa na kutwaa taji la Ligue 1.
Inasadikika kuwa Real Madrid wapo katika nafasi nzuri kuinasa saini ya Mbappe, ripoti zikidai kuwa klabu hizo mbili zimefikia makubaliano ya ada ya paundi milioni 161.
Manchester City pia imetajwa kwenye tetesi za kufikia dau sawa na Real Madrid, ingawa vyanzo kadhaa kutoka Etihad vimedai kuwa hakuna ukweli katika habari hizo.
Hata hivyo, L'Equipe limedai kuwa Arsenal hawajajitoa kwenye mbio za kumfukuzia kinda huyo nyota kutokana na uhusiano mzuri baina yake na Arsene Wenger.
Kulingana na hali ya kiuchumi ya Arsenal, hawataweza kuzifikia Madrid na Man City katika mbio hizo, kadhalika hawana fursa ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment