tuwasiliane

Tuesday, January 24, 2017

Pesa ya China yamnasa Olunga wa Kenya

Olunga

Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Michael Olunga ameingia katika orodha ya wanandinga walioamua kukimbila katika Ligi ya China.
Olunga, 23, aliyekuwa akikipiga katika klabu ya IF Djurgarden ya Sweden amesajiliwa na klabu ya Guizhou Zhicheng inayoshiriki Ligi Kuu ya China.
Kwa mujibu wa wakala wake Patrick Dark, dau  la uhamisho wa Olunga linatajwa kuweka rekodi kwa mauzo ya wachezaji kutoka Sweden.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Gor Mahia aliyewika katika mashindano ya Kombe la Kagame mwaka 2015 jijini Dar aling’aa katika msimu wake wa kwanza nchini Sweden kwa kufunga mabao 12 katika mechi za Ligi Kuu.
Anaungana na mshambuliaji wa Misri Al Ghazal aliyesainiwa huku akiwa mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kucheza katika ligi ya China inayokuja juu kwa kasi kutokana na uwekezaji mkubwa wa pesa unaofanywa na kampuni za China.

No comments:

Post a Comment