tuwasiliane

Tuesday, January 24, 2017

Mashabiki wa Togo wavunja nyumba ya kipa wao..Je, wataenda robo fainali.

togo
Hapo jana kundi B tulishuhudia mchezaji wa pili kati ya wale watatu bora Afrika Ryad Mahrez akimfuata Aubemayang nje ya mashindank ya Afcon.Algeria na Zimbabwe zimeaga rasmi mashindano.Leo kazi ipo tena kwani timu zote nne za Group B zina nafasi kwenda hatua inayofuata.Kupitia ZBC2 unazidi kuiona live Afcon2017.
Baada ya kufungwa na Morocco nyumba ya Kossi Agassa golikipa wa Togo ilivunjwa huko Togo,hii ilitokana na golikipa huyo kuonesha kiwango kibovu hali iliyowapelekea mashabiki wa timu yake kuwa na hasira.Na leo kuna hati hati akaukosa mpambano wao dhidi ya DR Congo.Kocha wao Claude Le Roy amesema habari za tukio ya nyumba ya Agassa kuvunjwa zimemuathiri sana.”Kama atahitaji kucheza ama hapana nitaheshimu maamuzi yake,amekasirika sana na kuathirika kiakili” aliongeza Le Roy.
Togo leo watahitaji kuwafunga DR Congo lakini huku wakiomba Ivory Coast wawafunge Morocco.Endapo Togo watawafunga DR Congo wenye pointi 4 nao watakuwa na pointi 4 sawa na Congo ila mmoja atafuzu kutokana na idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.DR Congo wenyewe wakicheza na kocha wao wa zamani Claude Le Roy watahitaji angalau suluhu ambayo watafikisha pointi 5 watafuzu hatua ya 8 bora kwani hata Morocco wakimfunga Ivory Coast,DR Congo watapeta wakiwa nafasi ya pili.
Ivory Coast mabingwa watetetzi wana pointi 2 tu hadi sasa,ushindi kwao ni lazima kama wanataka kuendelea katika robo fainali.Pointi 5 wakipata zitawahakikishia nafasi hiyo.Lakini sio kazi rahisi kwani kocha Herve Renard anataka kuonesha umwamba wake Afrika akihitaji kuchukua kombe la 3 la Afcon akiwa na nchi tatu tofauti.Na leo anajua kipigo kutoka kwa Ivory Coast kitawatoa mashindanoni.
Hakuna kulala leo kundi C,ni Morocco Ivory Coast,DR Congo au Togo anaeenda robo fainali?saa nne kamili usiku hakikisha hukosi ZBC2.


No comments:

Post a Comment