tuwasiliane

Monday, January 9, 2017

John Terry: Chelsea yapanga kukata rufaa kadi nyekundu

John Terry
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema klabu hiyo inatafakari uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa nahodha John Terry wakati wa mechi ya FA Jumapili.
Chelsea walilaza Peterborough 4-1 mechi hiyo.
Blues walipokuwa mbele 3-0, Terry, 36, alimwangusha mshambuliaji Lee Angol na refa Kevin Friend akaamua kuwa alikuwa mchezaji wa mwisho wa Chelsea.
"Lazima uheshimu uamuzi, lakini wakati huu labda tutakata rufaa," alisema Conte.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Terry kuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi tangu Oktoba.
Chelsea wakishindwa kwenye rufaa hiyo, basi Terry hatakubaliwa kucheza mechi ya Ligi ya Premia ugenini kwa mabingwa watetezi Leicester City tarehe 14 Januari.
John Terry ameoneshwa kadi tatu kati ya sita nyekundu walizoonyeshwa wachezaji wa Chelsea karibuni zaidi

No comments:

Post a Comment