tuwasiliane

Wednesday, December 14, 2016

Yaya Toure: Sikujua Coke ilikuwa imeongezwa pombe

Yaya Toure
Mchezaji nyota wa Ivory Coast Yaya Toure amesema hajapinga shtaka la kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, amesema kwamba hakunywa pombe makusudi alipokamatwa akiendesha gari akiwa mlevi.
Ameandika kwenye Facebook kwamba "inafahamika wazi kwamba mimi ni Mwislamu na huwa sinywi pombe."
Hata hivyo, hajaelewa ni vipi alijipata akinywa pombe ama akajipata akiwa amelewa bila yeye kufahamu.
Gazeti la The Mirror la Uingereza linasema kwamba alidai alikunywa Diet Coke na hakujua kwamba kwenye jagi aliyokuwa akitumia kunywa palikuwa pameongezwa kilevi aina ya brandi.
Gazeti hilo linasema amepigwa marufuku kutoendesha gari kwa miezi 18 na kupigwa faini ya $68,000 (£54,000).Mchezaji huyo wa Manchester City amesema: "Daima nimekuwa nikikataa pombe. Yeyote anayenifahamu na anayefuatilia uchezaji wangu atakuwa bila shaka ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kujitolea kwangu kuheshimu dini yangu."
"Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama kwamba sikunywa pombe makusudi. Jaji akinihukumu mwenye alikubali kwamba sikuwa nimekunywa pombe makusudi."
Amesema kesi yake ilihitimishwa Jumatatu na kwamba alikubali shtaka.
"Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikunywa pombe makusudi, nakubali marufuku na faini na naomba radhi kwa yaliyotokea," aliongeza.


No comments:

Post a Comment