tuwasiliane

Wednesday, December 14, 2016

SIMBA YAMSAJILI STRAIKA ALIYEIFUNGA YANGA


Katika kuendelea kukiboresha Kikosi chake Klabu ya Simba jana imemsajili mshambuliaji Pastory Athanas akitokea Klabu ya Stand United.
Pichani ni Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na mshambuliaji Pastory baada ya Kusaini rasmi kuitumikia klabu ya Simba.
mshambuliaji chipukizi Pastory Athanas aliyefunga bao pekee la Stand United katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
‘Dogo’ huyo wa umri wa miaka 22, aliipasua ngome ya Yanga Septemba 25 mwaka huu Uwanja wa Kambarage Shinyanga iliyokuwa chini ya Mtogo Vincent Bossou na kumtungua kipa Ally Mustafa ‘Bafrthez’ dakika ya 58. 

No comments:

Post a Comment