tuwasiliane

Wednesday, December 7, 2016

Sammy Lee ajiuzulu kama kocha msimamizi wa England.

Lee mwenye umri wa miaka 57, aliteuliwa kama msaidizi wa Sam Allardyce mwezi Julai
Sammy Lee amewacha wadhfa wake kama kocha msimazi wa timu ya England.
Lee mwenye umri wa miaka 57, aliteuliwa kama msaidizi wa Sam Allardyce mwezi Julai na kuendelea na jukumu hilo baada ya Allardyce kupigwa kalamu.
Lee aliendelea kuhudumu kama kocha msaidizi wakati Gareth Southgate alipokuwa akihudumu kama kaimu meneja wa England.
Southgate alisaini mkataba wa miaka minne na shirikisho la soka nchini Uingereza FA tarehe 30 Novemba na kuamua kumuacha nje Lee.
''Nilihisi kuna umuhimu kwa kuleta kikosi changu mwenyewe na Sammy aliheshimu uamuzi huo,''Southgate alisema.
Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Liverpool, alikuwa na wakati mfupi na klabu hiyo ya England, chini ya meneja Sven-Goran Eriksson mwaka wa 2005.
Alijiunga na Bolton,kwa muda mfupi alihudumu kama meneja wa Trotters mwaka 2007 kabla ya kurudi kama meneja msamizi wa Reds chini ya Meneja Rafael Benitez.
Lee alirudi Bolton mwaka 2012, kama mkuu wa chuo cha mafunzo na maendeleo,kabla ya kujiunga na kikosi cha mameneja wa Southampton mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment