tuwasiliane

Wednesday, December 21, 2016

Ratiba ya Yanga CAF Champions League

caf 1
Draw ya mechi za awali kuwania taji la ligi ya mabingwa Afrika imetoka leo, Tanzania inawakilishwa na Yanga ambao ndio mkabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.
Yanga imepangwa kucheza na Ngaya de Mbe ya Comoro katika mchezo wa awali ambapo Yanga itaanzia ugenini kabla ya kuja kucheza mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.
Endapo Yanga itaiondosha Ngaya de Mbe, iatasonga mbele na kukutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia vs APR ya Rwanda. Kama Yanga itapita katika hatua hiyo, itafuzu na kuingia katika hatua ya makundi.
Mechi za hatua ya awali zinatarajiwa kuchezwa February 10,11 na 12 2017 huku zile za marudiano zikitaraji kupigwa March 17,18 na 19, 2017.

No comments:

Post a Comment